Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mama Salma Kikwete afiwa na Baba yake mzazi



MKE wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum (CCM) amepata pigo kwa kuondokewa na baba yake mzazi, Mzee Rashid Mkwachu leo Alhamisi, Julai 19, 2018.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mjukuu wa marehemu ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, msiba huo upo nyumbani kwa Dkt. Jakaya Kikwete maeneo ya Msasani jijini Dar es Salaam na mazishi yatafanyika kesho Ijumaa, Julai 20, 2018 katika Makaburi ya Kisutu majira ya saa 10:00 jioni.



Pole sana mama salma kikwete, mungu amlaze mahali pema peponi baba yetu aliye tangulia mbele za haki[amin]

Comments