Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Ndugu Wabaini Ndugu yao Yupo Hai Baada Kukabidhiwa na Hospitali Akidaiwa Amekufa

Ndugu Wabaini Ndugu yao Yupo Hai Baada Kukabidhiwa na Hospitali Akidaiwa Amekufa

Ndugu wabaini binti yao yupo hai muda mfupi baada ya kukabidhiwa mwili wa binti huyo kwa hatua za mazishi ikiwa ni baada ya daktari kuthibitisha kifo chake

Binti huyo, Selina Michael(17) mkazi wa mtaa wa Butunga alipelekwa katika hospitali ya Baptist kupata matibabu na baadae familia kuarifiwa na Mganga wa zamu kuwa binti huyo amefariki

Wazazi wa binti huyo wameeleza kuwa chanzo cha binti huyo kupelekwa hospitali ni baada ya kuanguka ghafla alipokuwa akishuhudia vurugu zilizokuwa zikiendelea nyumba ya jirani

Aidha, Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali hiyo, James Chausa amekiri kumpokea binti huyo na kwamba Mganga wa zamu wa siku hiyo Cassian Ndilaliha alimpima na kubaini kuwa tayari amekwishapoteza maisha

Inadaiwa kuwa binti huyo alipoteza maisha kwa nguvu za giza na wakati daktari anampima hakuwa na mapigo ya moyo

Comments