Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Kamishna Magereza aeleza kiini msongamano wa wafungwa

Mbeya. Kamishna Jenerali wa Magereza, Juma Malewa amesema jeshi hilo linakabiliwa na msongamano wa wafungwa kutokana na kuongezeka vitendo vya uhalifu na makosa ya kijinai.
Dk Malewa amesema hayo leo Jumapili Desemba 31,2017 katika Gereza Kuu la Mkoa wa Mbeya akiwa ziarani kukagua magereza na kuzungumza na askari wa jeshi hilo.
Amesema msongamano unatokana na majengo yanayotumika kuwahifadhi wafungwa ni yaliyojengwa enzi za mkoloni.
Hata hivyo, amesema wamejipanga kuendelea kuongeza idadi ya magereza kwa kila wilaya licha ya baadhi ya wananchi kutopendezewa na jambo hilo.
“Wakati tunapata Uhuru watu tulikuwa kama 10 milioni, hadi sasa majengo kama yameongezeka basi ni mawili lakini ni yaleyale; pia kuna makosa mapya ya uhalifu yameongeza ambayo zamani hayakuwepo,” amesema.
Amesema makosa ya dawa za kulevya na utakatishaji fedha yamejitokeza; huku mauaji yakiongezeka.
Pia, amesema msongamano unasababishwa na kesi zinavyoendeshwa mahakamani ambako zipo zinazochukua muda mrefu upelelezi kukamilika.
Wakati huohuo, Dk Malewa amesema katika kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kuongeza uzalishaji wa chakula kwa lengo la kujitegemea ifikapo mwaka 2022 wametenga magereza 10 yatakayotekeleza mpango wa uzalishaji.
Amesema chakula kitakachozalishwa kitatumika ndani ya magereza hayo na kulisha Taifa litakapokabiliwa na uhaba.
“Kwa sasa Jeshi la Magereza linaitegemea Serikali kwa asilimia 100 ilhali ina rasilimali watu ya kutosha kuzalisha chakula. Hivyo, tumeanza utekezaji kwa magereza 10 na lengo ni hadi kufika miaka mitano ijayo tuwe tunajitegemea kwa asilimia 100 bila Serikali,” alisema Dk Malewa.

Comments

Popular Posts