Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Uongozi ni koti la kuazima, Makamba akumbusha wenzake

Waziri wa Mazingira na Muungano, January
Waziri wa Mazingira na Muungano, January Makamba 
Dar es Salaam. Waziri wa Mazingira na Muungano, January Makamba ameamua kutumia sehemu ya siku za mwisho wa mwaka kuwakumbusha wenzake kuhusu nyadhifa wanazoshikilia.
“Uongozi ni koti la kuazima,” ameandika waziri huyo wa Ofisi ya Makamu wa Rais katika akaunti yake ya Twitter jana, Kama ilivyo kwa watumaji wengi wa ujumbe mfupi katika mtandao huo, Makamba hakutaka kufafanua kauli yake zaidi ya kuthibitisha kuwa iko kwenye akaunti yake.
Makamba, mmoja wa makada walio katika Baraza la Mawaziri la pili baada ya kuingia kwa mara ya kwanza wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne, ni mmoja wa watu wanaotuma ujumbe mara kwa mara katika mtandao huo.
Katika ujumbe wa jana, Makamba ameandika: “Uongozi ni koti la kuazima. Kuna wakati utarudisha tu. Kama ulikuwa unawakoga nalo watu, likirudi unaadhirika.”
Pamoja na kutoa tahadhari hiyo, Makamba bado hajakumbana na adha ya kupoteza uongozi tangu aondoke Ikulu ambako alikuwa mwandishi wa hotuba wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne.
Baada ya kutoka Ikulu, mtoto huyo wa katibu mkuu wa zamani wa CCM, aligombea ubunge wa Bumbuli mkoani Tanga mwaka 2010 na kushinda na baadaye kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kabla ya kushika wadhifa wa sasa.
Hata hivyo, Makamba ameshuhudia mawaziri wenzake kadhaa wakipoteza nyadhifa zao na kuwa wananchi wa kawaida, wakiwamo walioenguliwa kutokana na kashfa kama za Tokomeza, Escrow, makinikia, Tanzanite na wengine walioachwa katika mabadiliko ya kawaida ya Baraza la Mawaziri

Comments

Popular Posts