Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mamia wajitokeza kumuaga Jaji Kisanga

Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini kitabu cha maombolezo na kutoa heshima ya mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. Robert Kisanga aliyefariki dunia tarehe 23 Januari, 2018 katika hospitali ya Regency Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameaga mwili wa Marehemu Jaji Kisanga nyumbani kwake Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Januari, 2018. 

Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria,Profesa Palamagamba Kabudi leo ameongoza mamia ya wakazi wa Dar es Salaam kuuga mwili wa Jaji Mstaafu Robert Kisanga aliyefariki mwanzoni mwa wiki hii.
Kabudi ameongoza mamia ya wakazi hao walioaga mwili ya Kisanga katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Msasani.
Viongozi wengine walioshiriki kuuaga mwili huo ni pamoja ni Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma, Mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Anna Mkapa na Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba, majaji na viongozi wa taasisi mbalimbali za serikali.
Kwa mujibu wa mjukuu wa marehemu, Fred Kisanga amesema mwili wa marehemu utazikwa katika kijiji cha Mbokomu, Mkoa wa Kilimanjaro

Comments

Popular Posts