Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mapingamizi yatupiliwa mbali Kinondoni


Dar es Salaam. Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Kinondoni ambaye pia mkurugenzi wa manispaa hiyo, Aron Kagurumjuli ameyatupilia mbali mapingamizi matatu yaliyowasilishwa na wagombea wa vyama vya Chadema, CCM na CUF.
Mapingamizi hayo ni kwa mgombea wa CUF, Rajab Juma kumwekea mgombea wa Chadema, Salumu Mwalimu, wakati Mwalimu yeye alimwekea Maulid Mtulia wa CCM na mgombea huyo wa chama tawala alimwekea mgombea wa SAU, Johnson Mwangosi.
Baada ya jana ofisi ya msimamizi wa uchaguzi kutoa barua ya utetezi kwa wagombea waliowekewa mapingamizi leo Jumanne imetoa majibu ya kuyatupilia mbali mapingamizi hayo.
Akizungumza na Mwananchi leo, Jumanne Januari 23, 2017, Kagurumjuli amesema “Tumeyatupilia mbali mapingamizi yao kwa sababu hayana mashiko, kilichobaki ni wagombea kwenda uwanjani wakapambane,” amesema msimamizi huyo.

Comments