Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mtuhumiwa uvamizi wa shule akamatwa kwa agizo la Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kukamatwa Ajay Chohan anayedaiwa kuvamia eneo la Shule ya Msingi Mapinduzi wilaya ya Kinondoni na kumiliki ardhi kinyume cha utaratibu.
Chohan amekamatwa leo Ijumaa Januari 26,2018 baada ya Makonda kutoa amri kwa mkuu wa polisi wa wilaya hiyo, muda mfupi baada ya kuzindua ujenzi wa ofisi za walimu wa shule hiyo.
Anadaiwa kumiliki kinyume cha utaratibu kiwanja kilichopo katika Kata ya Kigogo, Mtaa wa Mbuyuni.
Hata hivyo, Chohan ame eleza kuwa ana vielelezo vya umiliki wa eneo hilo kutoka serikalini.
Awali, mwalimu mkuu wa shule hiyo, Fina Mauki alimuomba Makonda kutafuta suluhu.
“Tuna tatizo la wananchi kuvamia maeneo ya shule na kujimilikisha kinyume cha utaratibu. Tunakuomba ukemee suala hili kwa kuwa ardhi ya shule iliyopo haitoshelezi mahitaji,” amesema Mauki.
Akijibu ombi hilo, Makonda amesema ujenzi wa ofisi za walimu wa shule za msingi Dar es Salaam utakwenda sambamba na kurudishwa mipaka ya awali ya shule husika.
Ametoa wito kwa wote waliovamia maeneo ya shule kuondoka kabla sheria haijachukua mkondo wake.
“Nimesikia eneo hili kuna mtu anadai ni la kwake, yuko  wapi huyo? Polisi mkamateni mara moja. Jambo hili lianze kuchunguzwa, haiwezekani suala hili la kuvamia maeneo ya shule tukaendelea kulifumbia macho,” amesema.

Comments

Popular Posts