Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Saudi Arabia na UAE zaanza kutoza kodi kwa mara ya kwanza
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionSaudi Arabia na Milki ya nchi za Kiarabu zaanza kutosa kodi kwa mara ya kwanza
Kodi ya bidhaa na huduma imeanza kutozwa kwa mara ya kwanza kabisa katika mataifa ya Saudi Arabia na Milki ya Nchi za Kiarabu.
Kodi hiyo ya asilimia tano itatozwa kwa bidhaa nyingi na huduma.
Mataifa ya Ghuba kwa miaka mingi yamewavutia wafanyakazi wa kigeni kwa ahadi kuwa hawatatozwa kodi.
Lakini serikali zinataka kuongeza kipato chao wakati bei za mafuata ziko chini.
Kodi hiyo ilianza kutekelezwa tarehe mosi Janauari mwaka huu katika nchi zote.
UAE inakadiria kuwa katika mwaka wa kwanza kipato kutoka kwa kodi kitakuwa dola bilioni 3.3.
Petroli, chakula, bili nyingine na vyumba vya hoteli sasa vitatoswa ushuru.
Mashirika yakiwemo la Fedha Duniani IMF kwa muda mrefu yamezitaka nchi na Ghuba kuacha kutegemea mafuta kwa pato lao.
Nchini Saudi Arabia asilimia 90 ya bajeti hutokana na mauzo ya mafuta huku UAE ikitegemea mafuta kwa asliimia 80.
Comments
Post a Comment