Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Tanzania kinara ukuaji wa Uchumi Jumuishi

Usimamizi mzuri na utekelezaji wa Sera mbalimbali za kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu kujenga na kumiliki uchumi, kumeifanya Tanzania kuibuka kinara miongoni mwa nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kuwa na Uchumi Jumuishi (Inclusive Economy) unaokua duniani.
Taarifa iliyotolewa na Word Economic Forum kupitia mradi wake wa mradi wa ‘The Inclusive Development Index’, imeitaja Tanzania kushika nafasi ya kwanza kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na ya 48 kati ya nchi 103 zilizofanyiwa tathmini ya nchi zenye Uchumi Jumuishi duniani,
Katika orodha ya kumi bora, nchi zilizofuatia na nafasi ziliyoshika kidunia ni pamoja na Ghana (52), Cameron (53), Burundi (55), Namibia (56), Rwanda (57), Uganda (59), Mali (60), Senegal (61) na Nigeria (63).

Takwimu za ukuaji huu zinaakisi moja kwa moja kauli ya Rais John Pombe Magufuli ambaye amekuwa akielezea kutaka uchumi wa Tanzania umilikiwe na wananchi kwa njia mbalimbali ikiwemo kutekeleza sera ya uchumi wa viwanda ambapo watanzania wengi hivi sasa wamekuwa wakitekeleza sera hiyo kwa kuanzisha viwanda vikubwa na vidogo.
Mtaalamu wa  masuala ya Uchumi na Mhadhiri wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Honest Ngowi amesema   takwimu zilizotolewa na taasisi hiyo zinatafsiri kuwa uchumi wa Tanzania unaelekea kumilikiwa na watu wengi zaidi.
Jambo ambalo litasaidia kupunguza pengo la kipato kati ya walionacho na wasionacho.
Profesa Ngowi ameeleza kuwa uchumi wa aina hiyo unawashirikisha wananchi kumiliki uchumi na kuwafanya watu wengi kufaidi matunda ya ukuaji wa uchumi wa nchi.
“Taarifa hizi ni njema kwani kitaalam tunaita broad based economy ambapo watu wengi wanashirikishwa kumiliki uchumi na wengi wanafaidi,” ameeleza Profesa Ngowi
Ameongeza kwamba  kuna nchi zingine zinauchumi mzuri lakini unamilikiwa na watu wachache na kufanya kuwa na pengo kubwa kati ya walionacho na wasionacho.
Katika siku za hivi karibuni, Taasisi mbalimbali duniani zimekuwa zikitoa ripoti zikiielezea Tanzania kupaa kiuchumi ambapo ripoti za Shirika la Fedha Duniani (IMF), Benki ya Dunia (WB) na Taasisi ya Goldman Sachs ya Marekani hivi karibuni zilitabiri kuwa wakati uchumi wa dunia utakua kwa wastani wa asilimia 3.0 hadi 4.0, ukuaji wa uchumi wa Tanzania unatajwa kuendelea kuwa kati ya nchi tano bora za Afrika ukitarajiwa kukua kwa asilimia 6.5 hadi 7.0 katika mwaka 2018.

Comments

Popular Posts