Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Tump ateta na Kagame, amtuma atoe salamu


Davos, Uswisi. Rais Donald Trump amemuomba Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika Paul Kagame kumpelekea "salamu za upendo" kwa viongozi wengine wa bara hilo, baada ya kulalamikiwa kuwa amewadhalilisha Waafrika.
Aidha, rais huyo wa Marekani mwenye maneno mengi amempongeza Rais Kagame kwa kuchaguliwa kwake kuongoza bara hilo jambo ambalo Trump amesema ni “heshima kubwa”.
"Najua baadaye utakwenda kwenye mkutano wako wa kwanza. Tafadhari nipelekee salamu zangu kwao," Trump alimwambia Kagame baada ya kukutana ana kwa ana leo kando ya mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) unaofanyika Davos, Uswisi.
Rais wa Marekani alikataa kujibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kuripotiwa msimamo wake wa kudharau nchi za Afrika kwa kuzifananisha na mashimo ya takataka akiita “mataifa machafu” alipokutana na viongozi wa wabunge kujadili suala la uhamiaji katika Ikulu ya White House.
Kauli hiyo ilisababisha shutuma kutoka kila kona duniani na baadhi ya viongozi wa Afrika walitaka maelezo kupitia mabalozi wa Marekani. Mataifa 55 wanachama wa AU chini ya aliyekuwa mwenyekiti wake Moussa Faki Mahamat yalimtaka Trump awaombe radhi Waafrika, ingawa Trump mwenyewe alikana kutoa matamshi hayo ila anakiri alitumia maneno makali.
Trump amesema alikuwa na "majadiliano ya kina" jijini Davos na Kagame, ambaye kwa upande wake alisema walikuwa "majadiliano mazuri" kuhusu uchumi na biashara.

Comments

Popular Posts