Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

VIDEO-Waliovamia Ngorongoro watakiwa kuondoka

Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangallah amezitaka kaya 83 zinazodaiwa kuvamia eneo la serikali la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kujiandaa kuondoka.
Akizungumza na waandishi leo Januari 28 baada ya kutembelea eneo hilo la Njiro, Kigwangallah amesema ana taarifa viwanja hivyo waliuziana maafisa wa Serikali  bodi la Utalii na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kinyume cha sheria.
"Katika eneo tumepewa taarifa waliopewa viwanja  wapo mawaziri wakuu wastaafu wawili ,viongozi wa serikali wastaafu na tayari tumewasiliana na Waziri wa ardhi kupata nyaraka zao" amesema
Katika eneo hilo, kuna nyumba za wakuu kadhaa wa mikoa wastaafu, viongozi wa taasisi za serikali wastaafu na wafanyabiashara kadhaa.
Awali Meneja wa huduma za sheria wa Ngorongoro, Egudius Mweyunge amesema  NCAA ilinunua eneo hilo mwaka 2006 kutoka tume ya ubinafsishaji mashirika ya umma(PSRC) mwaka 2006 ekari 40 kwa Sh1.8bilioni.
Hata hivyo amesema baada ya kutaka kuendeleza eneo walikuta tayari halmashauri ya jiji la Arusha wamegawa viwanja 83 tangu mwaka 1996.
"Tulipowafuata jiji wakakiri wamefanya makosa na watatufidia eneo jingine lakini tumeshindwa kufikia muafaka" amesema Meneja huyo
Awali Mhifadhi mkuu wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Dk Fredy Manongi amesema eneo walilovamiwa ni  mali ya NCAA na wana mikakati ya kuwekeza.



Comments

Popular Posts