Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Wabunge Chadema wataka Mollel asichaguliwe

Siha. Wabunge wa viti maalumu (Chadema), Lucy Owenya na Cecilia Pareso wamewataka wananchi wa Jimbo la Siha kutomchagua mgombea wa CCM, Dk Godwin Mollel.
Awali Mollel alikuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema lakini Desemba 14 mwaka jana alijiunga CCM na anagombea tena nafasi hiyo kupitia chama tawala.
Wabunge hao walitoa ombi hilo leo Januari 26, mwaka 2018 katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika kijiji cha Ngarenairobi na kuwataka wananchi wamchague mgombea wa Chadema, Elvis Mosi.
Wamesema Dk Molell aliwaomba wananchi hao wamchague kuwa mbunge katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kwamba walimpa heshima hiyo wakati akiwa Chadema, lakini alijiuzulu na kutimkia chama kingine.
Uzinduzi wa kampeni hizo unaongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Comments

Popular Posts