Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Wanasiasa, viongozi wa Serikali wapewa angalizo

Dar es Salaam. Wanasiasa na viongozi wa Serikali wametakiwa kuhamasisha amani kwa kuwa ndiyo msingi utakaoifanya Tanzania kuendelea kuwa tulivu.
Wito huo umetolewa leo Jumatatu Januari Mosi, 2018 na msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Chediel Lwiza baada ya kumalizika ibada ya Mwaka Mpya katika Usharika wa Azania Front jijini Dar es Salaam.
Lwiza amesema viongozi wana nafasi kubwa ya kuhakikisha amani inaendelea kuwepo nchini.
"Amani ndiyo msingi wa kila kitu hakuna kitakachofanyika kama hakuna amani, tuidumishe. Kwa zile nchi ambazo zimeshaingia kwenye machafuko nawasihi kuwa njia pekee ya kuirudisha amani ni kukaa kwenye meza ya majadiliano," amesema.
Kauli hiyo haikupishana na aliyoitoa mmoja wa washarika, Frederick Minja ambaye amesisitiza amani akisema, "Tumeanza mwaka hatujasikia matukio ya ajabu, ni imani yangu kuwa amani imetawala basi tufanye kila linalowezekana iendelee kuwepo."

Comments