Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Wizara yatoa miezi mitano kwa TBA kukamilisha ujenzi


Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali mstaafu, Projest Rwegasira ametoa miezi mitano kwa Wakala wa Majengo (TBA) kukamilisha ujenzi wa nyumba za askari wa Jeshi la Magereza zilizoko Ukonga jijini Dar es Salaam.
Ametoa agizo hilo leo Ijumaa Januari 26,2018 alipofanya mazungumzi na maofisa wa TBA na wa Jeshi la Magereza baada ya kukagua ujenzi huo.
“…fanyeni juu chini mhakikishe mradi huu unakamilika ndani ya miezi hiyo mitano mliyosema. Ongezeni nguvu ili mkamilishe mradi huu kwa wakati,” amesema katika taarifa iliyotolewa na wizara.
Fedha za ujenzi wa nyumba hizo unaogharimu  Sh10 bilioni zilitolewa na Rais John Magufuli baada ya kufanya ziara Ukonga mwishoni mwa mwaka 2016.
Ujenzi ulianza mwaka jana badala ya Desemba 19, 2016.

Comments

Popular Posts