Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mbunge ataka mawaziri watembelee majimbo

Mbunge wa Kavuu (CCM) Dk Pudensiana Kikwembe amewavaa mawaziri na manaibu waziri kwa kuomba mwongozo wa kazi na wajibu wa mawaziri.
Mara baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni Dk Kikwembe
aliomba mwongozo wa Spika kuhusu kazi na wajibu wa mawaziri.
Amesema  mara nyingi wabunge wakati wa kuuliza maswali ya nyongeza
wamekuwa wakiomba kuongozana na mawaziri kwenda majimboni mwao.
“Naomba mwongozo wako Mwenyekiti nipate kujua wajibu wa mawaziri
nikuombwa na wabunge kwenda majimboni ama ni wajibu wao kuzunguka
majimboni kujua masuala na matatizo ya wananchi?”amehoji.
Amesema  hata mbunge anapokuwa jimboni wamekuwa wakipita na misururu ya
magari huku wananchi wakiwaona badala ya kusimama na kujibu hoja na
kero za wananchi.
“Kwa mfano mheshimiwa Kalemani (Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani)
ametoka Inyonga akapita Kavuu usiku… Lakini wakumbuke (mawaziri) kuwa
wao ni wabunge na wanaenda kusikiliza kero za wananchi hawaendi
kumsikiliza mkuu wa mkoa wala DC (mkuu wa wilaya),”amesema .
Amesema wanaofanya hivyo ni mawaziri wengi tu lakini akawataja baadhi
yao mbali na Kalemani ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na
Wazee (hakumtaja jina) ambaye alikwenda kukagua ujenzi wa zahanati
baada ya kuitwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda.
Mwongozo huo pia uliombwa na Mbunge wa Tanga Mjini (CUF) Mussa Mbarouk
amesema kuwa wakati wa Bunge mawaziri wamekuwa wakiwaahidi kuwa
wataongozana na wabunge kwenda majimboni lakini wakiwapigia simu baada
ya bunge kumalizika hawapokei.
“Mimi nataka kila waziri kabla yua bunge kumalizika atoe orodha yake
ataongozana na mbunge yupi kwenda jimboni kwasababu sasa wamekuwa
wakitudanganya. Watayarishe orodha zao kati ya mbunge wa kwanza hadi wa
mwisho watakayekwenda naye jimboni,”amesema.
Akijibu miongozo hiyo Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge amesema kanuni
hazikatazi waziri kuongozana na mbunge anapoombwa kufanya hivyo.
“Kutembelea maeneo mbalimbali ya nchi kuangalia utekelezaji wa ilani
ya CCM hilo ndilo jukumu wanapaswa wafanye hivyo sio baada ya
invitation (mialiko),”amesema.
Amesema kama waziri ametoa ahadi kwa mbunge bungeni kuwa ataongozana
naye kutembelea jimboni kwake si uungwana kutoonekana.
“Yale yanaoumizwa ni pale unapokwenda katika jimbo hata kwa kuitwa na
mtu mwingine na mbunge wa jimbo yuko bila hata kuwajulisha. Serikali
ikiweka utaratibu mzuri hakuna tatizo ili mbunge wa jimbo hilo
atambulike kwamba yeye ndiye yuko pale,”amesema.

Comments