Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mkapa aongoza mapokezi mwili wa Kingunge

Mwili wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru umepelekwa nyumbani kwake Victoria, Kijitonyama utakakolala.
Mwili wa Kingunge umepelekwa nyumbani leo Jumapili Februari 4,2018 jioni. Ulikuwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa  Muhimbili (MNH).
Wakati mwili wa Kingunge ukifikishwa nyumbani, baadhi ya viongozi waliokuwepo ni Rais mstaafu Benjamin Mkapa na mkewe Anna; Spika mstaafu Anne Makinda; Jaji mstaafu Joseph Warioba; Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Stephen Wasira na Balozi Getrude Mongella.
Baada ya mwili kupokewa, uliingizwa ndani ambako kwa mujibu wa kamati ya mazishi kutafanyika shughuli za mila pamoja na sala. Mwenyekiti wa kamati ya mazishi, Omary Kimbau amesema kesho Jumatatu Februari 5,2018 asubuhi itakuwa fursa kwa waombolezaji kufika nyumbani hapo kwa ajili ya taratibu za mazishi, kupata kifungua kinywa na kutafanyika misa.
Kimbau amesema saa sita mchana, mwili wa marehemu Kingunge utawasili katika viwanja vya Karimjee ambako kutafanyika shughuli ya kuuaga na saa tisa alasiri msafara wa kwenda makaburi ya Kinondoni utaanza na mazishi yanatarajiwa kufanyika saa 11:30 jioni.
Mwisho.

Comments