Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mrithi wa Kabila kujulikana Julai

Kinshasa, RD Congo. Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (RD Congo), Lambert Mende amesema Rais Joseph Kabila hana nia ya kugombea tena na atamtangaza Julai mwaka huu mtu ambaye ni chaguo lake wa kushindana katika uchaguzi wa Desemba
Msemaji huyo aliongeza kwamba Kabila anatarajia kuheshimu katiba na nguvu za kuachia madaraka baada ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba.
Akizungumza na Shirika la Utangazaji la VoA Idhaa ya Kifaransa akiwa Afrika Kusini, Mende alisema licha ya kuchelewa kumalizia usajili wa wapigakura katika maeneo ya vijijini serikali inaendelea kusimamia uchaguzi kulingana na ratiba iliyowekwa na tume ya uchaguzi.
Kwa mujibu wa Katiba ya RD Congo, Kabila hawezi tena kuwania muhula wa tatu wa urais.
Kabila ametawala tangu Januari 2001, siku chache baada ya mauaji ya baba yake Laurent Kabila. Aligombea rasmi na kuchaguliwa kuwa rais mwaka 2006 na akachaguliwa tena kwa kipindi cha pili mwaka 2011.
Lakini alikataa kung’atuka mwishoni muhula wake Desemba 2016. Uchaguzi unaotarajiwa kumpata mrithi wake umekuwa ukiahirishwa mara kwa mara, hali iliyoshawishi wapinzani kumshutumu kwa kuchezea mchakato ili azidi kuendelea kukaa madarakani, shutuma ambazo anakanusha.
Chini ya makubaliano yaliyosimamiwa na kanisa kati ya Kabila na wapinzani wake, rais alipaswa kung’atuka mwishoni mwa mwaka jana na kutengeneza mazingira ya uchaguzi wa mapema mwaka 2018. Lakini Kabila alikiuka mpango huo akasukuma uchaguzi hadi mwishoni mwa mwaka 2018.

Comments