Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Rais Magufuli atoa Sh2milioni kusaidia ujenzi wa Kanisa Chato

Rais John Magufuli akizungumza na waumini waRais John Magufuli leo Jumapili Februari 25, 2018 ameungana na waumini wa Parokia Teule ya Mlimani iliyopo Chato mkoani Geita kusali ibada ya dominika ya pili ya Kwaresma huku akichangia Sh2milioni kwa ajili ya ujenzi unaoendelea kanisani hapo.
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa leo Februari 25, 2018 na mwandishi wa habari msaidizi wa Rais, Emmanuel Buhohela imesema Parokia Teule ya Chato imepandishwa hadhi kutoka kilichokuwa Kigango cha Mlimani na hivi sasa waumini wanaendelea kukamilishja majengo ikiwemo nyumba ya Paroko kabla ya kusimikwa rasmi kuwa Parokia.
Akitoa salamu baada ya ibada hiyo, Rais Magufuli amewapongeza waumini wa parokia hiyo kwa juhudi walizofanya kujenga Kanisa la Parokia hiyo.
Katika taarifa hiyo, Rais amemshukuru Askofu wa Jimbo Katoliki Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi kwa kukipandisha hadhi kigango cha Mlimani kuwa Parokia.
“Pamoja na kujenga parokia yetu tuendelee kuliombea Taifa letu na kujiweka tayari katika maisha ya duniani,” amesema Rais Magufuli.
Ibada hiyo imeongozwa na Paroko msaidizi, Alex Bulandi na kuhudhuriwa pian na Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani.

Comments

Popular Posts