Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

VIDEO-Zitto ataka mkutano wa maridhiano nchini

Kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe ametaka kuitishwa mkutano wa kitaifa wa maridhiano ya kisiasa, kuundwa tume huru ya kuchunguza matukio ya ukiukwaji wa haki za binaadamu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha jana akiwa katika ziara ya kutembelea kata ambazo zina madiwani wa chama chake, alisema mkutano huo utajadili changamoto zote za uendeshaji siasa nchini.
Alisema ni muhimu kujadiliwa hali ya kisiasa nchini, kukubaliana kanuni za demokrasia ya vyama vingi kwa maelezo kuwa mfumo wa vyama vingi nchini upo hatarini.
“Katika mkutano huu, tunaomba kushirikisha asasi za kiraia, vyama vya wafanyakazi, wafanyabiashara, wakulima na wafugaji,” alisema.
Alisema yanayotokea katika siasa kwa sasa si ya kuwaachia wanasiasa pekee kwa maelezo kuwa yanahusu uhai wa watu wengine wasiojihusisha na siasa.
“Mkutano huu utoe maazimio ya kufanya mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa siasa ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi. Mabadiliko makubwa ya Jeshi la Polisi ili kulifanya lifanye kazi ya kulinda raia pamoja na mabadiliko ya Usalama wa Taifa ili kulinda Katiba,” alisema.
Kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu, Zitto alisema iundwe tume huru ya kuchunguza matukio yote ya mauaji ya raia.
“Tume ichunguze matukio ya kushambuliwa viongozi wa kisiasa na hata majaribio ya kuua baadhi ya wabunge ambao wengine sasa wapo hospitali wakiendelea na matibabu,”alisema.
Alisema licha ya kuwepo tume ya haki za binadamu kwa sasa haina makamishna na kubainisha kuwa kuna haja ya kushinikiza uchunguzi huru wa kimataifa chini ya umoja wa mataifa.
Zitto alisema Tanzania inaendeshwa na demokrasia ya mfumo wa vyama vingi hivyo ni wajibu wa kila raia kuulinda mfumo huu kwani una faida kubwa kwa nchi.
“kulinda Demokrasia yetu ni kulinda Katiba kwa kuwa kuna dalili zote za kurudishwa katika mfumo wa chama kimoja , umefika wakati watanzania wasimame na kuilinda katiba,” alisema.
Akizungumzia alichogundua kwenye ziara yake, alipendekeza ufanyike uchunguzi huru wa namna rasilimali za kibajeti za nchi zinavyogawanywa kati ya mijini na vijijini.
“hii ni kutokana na ukweli kuwa maisha ya wananchi vijijini ni mabaya mno hasa kukosa huduma za msingi kabisa kama maji, barabara, elimu na afya ilhali kuna miradi mikubwa mijini,” alisema.

Comments

Popular Posts