Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri autaka mgodi kuwalipa fidia wananchi 133

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amemtaka mmiliki wa mgodi wa dhahabu wa Nyarugusu kuwalipa fidia haraka wananchi 133 ambao mazao yao yameathiriwa na sumu na endapo atashindwa Serikali itafunga mgodi huo.
Wananchi wanaodai fidia ya mazao wamefunga barabara inayoelekea katika mgodi huo kwa siku nane sasa wakishinikiza kulipwa fidia ya Sh202.7milioni kama ilivyotangazwa na mtathimini wa Serikali, Bahati Albert Januari 17, 2018.
Madai hayo yanatokana na sumu iliyoingia kwenye mashamba ya wananchi baada ya kupasuka kwa shimo la maji ya sumu katika mgodi huo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Novemba 20, 2017 na kuathiri eneo lenye ukubwa wa ekari 273 zilizokuwa zimepandwa
mahindi, mpunga na maharage.
Wakizungumza na Nyongo jana Februari 24, 2018 alipotembelea eneo walilofunga barabara, baadhi ya wananchi hao Mashauri Kahengele na Pili Ramadhani wamedai licha ya Serikali ya wilaya kuwataka wafungue akaunti ya benki ili walipwe, hadi sasa hakuna utekelezaji.
Mkurugenzi mtendaji wa mgodi huo, Alex Kindersley amesema kuna upungufu uliojitokeza kwenye tathmini na kutaka urekebishwe jambo ambalo Nyongo amelipinga na kubainisha kuwa tathmini iliyofanywa na Serikali ni sahihi na anapaswa kuwalipa wananchi hao haraka.

Comments

Popular Posts