Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Wizara ya Afya yakiri kurudi homa ya Dengue D’Salaam


Wakati Serikali ikitangaza kuwapo kwa wagonjwa walioonyesha dalili za ugonjwa wa homa ya Dengue, hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam zimeeleza kuwa bado hazijapokea mgonjwa wa aina hiyo hadi sasa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya alisema kuwa ugonjwa huo upo huku akisema maelezo zaidi yatatolewa na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Kambi.
“Ni kweli jana nilitoa taarifa lakini Mganga Mkuu ana taarifa zaidi na yupo katika nafasi nzuri ya kulizungumzia hasa kwa kuangalia idadi ya kesi na mambo mengine,” alisema.
Hata hivyo, licha ya kuthibitisha kuwapo kwa maradhi hayo, Profesa Kambi alisema atatoa taarifa kamili kuhusu idadi ya waliougua leo.
Dk Ulisubisya alinukuliwa na gazeti moja la kila siku nchini akisema kuwa ugonjwa huo tayari umeingia tena nchini na tayari wagonjwa kumi na moja Jijini Dar es Salaam wameshaonyesha dalili za kuwa nao.
Dk Ulisubisya alisema wagonjwa hao wamebanika katika vituo viwili vya afya, IST na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road(ORCI).
Alisema tayari Wizara kwa kushirikiana na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), wanaendelea na uchunguzi kubaini kama kuna wagonjwa wengine zaidi.
Hata hivyo, waganga wakuu wa Hospitali za Temeke, Amana na Mwananyamala walipotafutwa kuzungumzia uwapo wa ugonjwa huo walisema hawajapokea wagonjwa.
Dk Meshack Shimwela wa Amana alisema hospitali hiyo haina taarifa za ugonjwa huo.
Mganga Mkuu wa Temeke, Amani Malima alisema hana taarifa lakini aliahidi kufuatilia kama mgonjwa yeyote aliyefikishwa hospitalini.
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mwananyamala, Daniel Nkungu kadhalika alisema hawajapokea mgonjwa yeyote hadi jana.
Dengue
Kwa mara ya kwanza ugonjwa huo ulilipuka nchini mwaka 2014 na watu 400 waliugua huku watatu wakifariki dunia akiwamo Dk Gilbert Buberwa (36) aliyekuwa mtaalamu wa tiba katika Hospitali ya Temeke.

Comments

Popular Posts