Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Halima Mdee akamatwa saa tisa usiku



 Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee.

Mdee amekamatwa leo alfajiri uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini Afrika Kusini inakoelezwa alilazwa kwa matibabu.

Akizungumza   leo Aprili Mosi, 2018, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema ambaye pia ni Meya wa Ubungo, Boniface Jacob amesema, "Ni kweli amekamatwa leo Saa 9 alfajiri  Airport, akitokea Afrika Kusini alipokuwa amelazwa kwa matibabu na sasa yupo Central."

Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) huenda akaunganishwa na vigogo wengine sita akiwamo Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe katika kesi inayowakabili.

Vigogo hao wengine tayari wamekwisha kupandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa mashtaka nane.

Kukamatwa kwa Mdee kunafikisha watuhumiwa saba kati ya nane  ambao wamekwisha kuhojiwa mwingine ambaye bado na huenda anatafutwa na jeshi hilo ni mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.
Hata Hivyo baada ya kupigiwa simu kamanda wa polisi kanda maalum, Lazaro Mambosasa simu yake haikupokelewa.

Comments