Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Katibu Mkuu Chadema azungumzia Muungano



Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashini amesema ni muhimu kuwa na muungano wenye afya katika maendeleo na ustawi wa Watanzania badala ya kujadili kama uwepo au usiwepo.
Dk Mashinji amesema hayo jana akiwa mkoani Mtwara mara baada ya kutoka katika Mahakama ya Wilaya ya Mtwara katika kesi inayomkabli mbuge wa jimbo la Ndanda, (Chadema) Cecil Mwambe.
 “Watu wote makini duniani wanaungana, hata kama siyo kuungana tu kisiasa wanaungana kiuchumi, hata kama siyo kuungana kiuchumi wanaungana kijami kwa hiyo hatuongelei suala la uwapo au usiwapo tunachokiongelea hapa huu Muungano uwepo kwa sura gani,”amesema Mashinji.
“Chama chetu kinaamini kabisa ni Muungano wa nchi mbili ni lazima uchukuliwe katka mazingira ambayo nchi mbili ziliungana...lazima kuwe na maridhiano,”ameongeza.
Amesema kuna nchi ziliungana kama United Kingdom, Scotland, England na Marekani na hivyo Tanzania inaweza kujifunza kuhakikisha wanaungana bila kuhitalafiana.
“Suala Muungano lina changamoto zake nyingi lakini hapa hatujadili kuungana au kutoungana na wala Chadema haijadili kuungana au kutoungana,Chadema inajadili ni jinsi gani tutakuwa na Muungano wenye afya katika maendeleo na ustawi wa watanzania.”amesema Dk Mashinji

Comments

Popular Posts