Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

‘Mahakimu fuateni sheria wakati wa kutoa ushahidi’



Mahakimu wa mahakama za wilaya Zanzibar wametakiwa kufuata taratibu za kisheria zinazotoa haki kwa watoto katika utoaji wa ushahidi.
Mwenyekiti wa mahakama za watoto visiwani hapa, Neyla Abdallah alitoa ushauri huo jana wakati wa warsha maalumu iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Zanzibar na kuwakutanisha mahakimu na watetezi wa haki za wanawake na watoto.
Alisema kwamba kumekuwapo na malalamiko kwa baadhi ya familia wanaofika mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa kesi kuwa kuna ukiukwaji wa taratibu za haki za mtoto hasa wanapotakiwa kutoa ushahidi.
Neyla alisema kwamba ni vyema mahakimu kutambua kuwa mtoto ni tofauti na mtu mzima, hivyo wana wajibu wa kuandaa mazingira maalumu ili watoto hao waweze kutoa ushahidi kwa usiri na kulinda haki zao.
“Kila hakimu inampasa kujitathmini kwanza kabla ya kusikiliza kesi hizi za watoto ikiwamo kutoa haki zao za msingi sambamba na kusikilizwa kwenye vyumba maalumu ambavyo ni tofauti kabisa na kumbi za wazi za mahakama kama ilivyozoeleka,” alisema.
Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe mjini hapa, Ally Abrahman alisema baadhi ya mahakimu wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utendaji wao wa kazi ikiwamo namna ya kuwalinda watoto waliolawitiwa au kubakwa.
Alisema iwapo mafunzo ya aina hiyo kwa mahakimu yataendelea kutolewa kila baada ya muda, changamoto hizo zitamalizwa kabisa na hatimaye haki za watoto kwenye mahakama zitazingatiwa.
Naibu Mrajisi wa Mahakama Kuu Zanzibar, Salum Hassan alisema imefika wakati kwa mahakimu kuzingatia na kufuata taratibu na sheria zinazomlinda mtoto katika kutoa ushahidi.
Alisema si jambo jema kuona baadhi ya mawakili wanasemwa vibaya na jamii kwa kukiuka taratibu za Mahakama.
Pia, aliitaka jamii kuacha kulalamika pembeni wanapokutwa na matatizo ya aina hiyo, badala yake wafike katika vyombo vya juu zaidi kutoa taarifa.

Comments

Popular Posts