Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mbowe ‘atokezea kivingine’ Kisutu


Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ambaye amelala mahabusu kwa siku tano, ameonekana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiwa ‘ametokezea kivingine’.
Tofauti na alivyozoeleka kuonekana, Mbowe ameonekana leo Jumanne akiwa na ndevu ‘nyeupe’ pamoja na suti za kawaida za chama hicho, zenye rangi ya kaki.
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Wilbard Mashauri alitaka Mbowe na wenzake watano kufikishwa mahakamani hapo leo Aprili 3,wakiwa na wadhamani wawili kila mmoja.
Washtakiwa hao walitakiwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh20 milioni na kuwa na barua kutoka kwa viongozi wao ama wa vijiji au mtaa, ambao watapaswa kuwa na nakala za vitambulisho vyao.
Kufuatia uamuzi huo uliotolewa Alhamisi, viongozi hao walijikuta wakila Sikukuu ya Pasaka wakiwa mahabusu.
Awali, Hakimu Mashauri alieleza dhamana kwa washtakiwa hao iko wazi, jambo ambalo lilipingwa na upande wa Serikali.

Comments