Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mbowe, wenzake wakamilisha masharti ya dhamana


Dar es Salaam. Viongozi sita wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wamekamilisha masharti ya dhamana.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imejiridhisha na nyaraka walizoziwasilisha wadhamini kwa ajili ya dhamana ya washtakiwa hao na imewakubalia kuwadhamini huku ikiwapa maelekezo kuhakikisha kuwa wanapatikana mahakamani kila wanapohitajika.

Masharti ya dhamana yao ni kusaini bondi ya Sh20 milioni  kuwa na wadhamini wawili wenye barua kutoka ofisi za Serikali za mitaa au vijiji na kuripoti kituo kikuu cha Polisi kila Alhamisi.


Mbali ya Mbowe wengine ni Katibu Mkuu Dk Vicent Mashinji, manaibu katibu wakuu John Mnyika (Bara), Salum Mwalimu (Zanzibar), Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake wa chama hicho, Ester Matiko wanakabiliwa na kesi ya jinai, wakidaiwa pamoja na mambo mengine ikiwamo kufanya mikusanyiko na maandamano yasiyo halali.

Wamekuwa mahabusu tangu walipopandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka hayo Machi 27 mwaka huu, 2018.

Comments