Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mdee kuunganishwa na vigogo wengine wa Chadema


Dar es Salaam. Wakati vigogo sita wa Chadema wakiwasili mahakamani, Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi, ameomba kufanya marekebisho ya hati ya mashtaka ili kumuunganisha Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.
 Mdee alikamatwa jana katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere(JNIA) akitokea Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa.
 Awali, viongozi sita wa Chadema, akiwamo Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, walisomewa mashtaka manane, yakiwamo ya uchochezi na kuhamasisha maandamano.
Lakini Mdee hakujumuishwa katika hati hiyo ya mashtaka  na hivyo Wakili Nchimbi ameiomba leo Aprili 3, kumuunganisha Mdee katika kesi hiyo.
Viongozi hao walitakiwa kuwa huru kwa dhamana tangu Machi 29 lakini wakaendelea kubaki mahabusu   baada ya kushindwa kusaini bondi ya Sh20 milioni.
Machi 29,  Hakimu Wilbard   Mashauri aliamuru kuwa viongozi hao wafikishwe mahakamani leo na kusaini bondi hiyo ndipo suala la rufaa lifanyiwe kazi.

Comments