Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

VIDEO-Mbunge azichambua ndege za Tanzania

Dodoma. Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali amesema ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kutoa huduma za usafiri wa anga asubuhi hadi jioni na kusitishwa usiku hakiwezi kulinufaisha shirika hilo, huku akifananisha kitendo hicho na huduma za usafiri wa daladala.
Akizungumza jana jioni Aprili 24, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mwaka 2018/19, Bobali amesema hakuna anayepinga shirika hilo kufufuliwa lakini tatizo ni uamuzi wa Serikali kununua ndege bila kuboresha miundombinu na kuwa na mipango endelevu.
“Tunapaswa  tuelewane hakuna anayekataa wala kupinga ATCL kufufuliwa. Tunachopenda kushauri ni namna na njia inayotumika kulifufua shirika. Mawaziri mpo hapa mnasoma ripoti mbalimbali za mashirika ya anga ya kimataifa na mnajua nini kinaendelea kwenye mashirika ya ndege mengine,” amesema.
“Kwa sasa takwimu zilizopo, kwa mwaka mmoja mashirika ya ndege duniani yanapata hasara ya Dola 8 bilioni za Marekani, kwa Afrika pekee mwaka uliopita mashirika ya ndege yalipata hasara ya Dola 600 milioni za Marekani. Ikiwa hali ndio hii tukienda kuifufua ATCL lazima tuwe na tahadhali.”
Amesema katika mjadala huo, baadhi ya wabunge wamehoji kitendo cha ndege za ATCL kutoa huduma, huku viwanja vya ndege nchini vikiwa vibovu na hakuna usafiri wa usiku wa ndege.
“Wakati tunanunua ndege tulijua tunasafiri nje ya nchi, lakini najua kusudio la kununua ndege ni zitumike ndani, kwanini zaidi ya viwanja vya ndege asilimia 70 nchini havina taa?” amehoji.

Comments

Popular Posts