Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Bilago azikwa kijijini Kasuga



Kigoma. Mwili wa aliyekuwa mbunge wa Buyungu (Chadema), Kasuku Bilago umezikwa katika makaburi ya kijiji cha Kasuga wilayani Kakonko, Kigoma leo.
Wakazi wa Kasuga alipozaliwa marehemu walianza kushiriki misa katika Kanisa Katoliki Kigango cha Kasuga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu kabla ya kuelekea makaburini kwa maziko.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Kigoma, Shaaban Madede amezungumza leo Mei 31, 2018 kuwa Bilago  atakumbukwa kwa utendaji wake uliotukuka na ukarimu.
Vilio na simanzi vilitawala wakati mwili huo ulipowasilishwa kanisani na baadaye makaburini.
Wengi walimzungumzia marehemu kama mtu aliyekuwa akiishi maisha ya kijamaa na wananchi wa jimbo lake la Buyungu na kila sehemu aliyofanya kazi.
Marehemu Bilago aliwahi kuwa mwalimu na baadaye Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika mikoa ya Kigoma, Rukwa na Mbeya.

Comments

Popular Posts