Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

CUF wajipanga mkutano mkuu



Naibu Mkurugenzi wa Mipango wa Chama cha Wananchi (CUF) Nassor Seif upande unaomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba, amesema wapo kwenye mchakato wa kufanya mkutano mkuu kwa ajili ya kupata viongozi wapya.
Seif alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na baada ya kuulizwa kuhusu madai ya chama hicho upande wa Lipumba ambaye ni mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, kufanya mkutano mkuu huku kikikabiliwa na mvutano wa uongozi uliosababisha kufunguliwa kesi mahakamani.
Alisema CUF kupitia Baraza Kuu, wanachosubiri ni kukutana pamoja na kutoa taarifa rasmi ya kufanyika kwa mkutano huo.
Alipoulizwa kuhusu wajumbe watakaoshiriki mkutano huo alisema kila kitu kinakwenda vyema na kusisitiza wajumbe halali wapo.
“Wajumbe wa mkutano mkuu wa Taifa watakapopata taarifa ya wito wa mkutano wasisite kujitokeza kwa lengo la kutimiza haki yao ya kikatiba. “Sisi tunafanya haya kwa mujibu wa katiba ya chama na ndiyo maana tumekuwa tukibarikiwa kila hatua na wenye kujua ukweli sasa wameanza kutuunga mkono,” alisema Seif.
Alipoulizwa kuhusu mkutano huo, Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Uhusiano wa Umma, Salim Abdallah Bimani upande wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alisema chama kipo imara na hakuna mjumbe atakayejitokeza kushiriki mkutano unaoitishwa na upande wa Lipumba.
Alisema wanaoratibu mipango ya mkutano huo wanaonyesha dalili za kuishiwa kisiasa na kuwataka wana CUF kuwapuuza.

Comments

Popular Posts