Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Ndugu waususa mwili wa anayedaiwa kufariki mikononi mwa Polisi



Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto 

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto  

Dodoma. Familia ya Mapunda wa Mtera wilayani Mpwapwa wameususa mwili ndugu yao Simon Mapunda (24) wakidai ameuawa na polisi wa kituo cha Mtera.
Simoni alikamatwa na polisi mmoja mchana wa Mei 26 kwa kile kilichoelezwa alikuwa na ugomvi na kijana mwenzake.
Msemaji wa familia Msafiri Gondwe alisema kuwa polisi walimkamata Mapunda wakimtaka akatoe maelezo kituoni ingawa ugomvi wao ulishasuluhishwa.
“Tuliomba kumuwekea dhamana, lakini polisi walikataa, siku hiyo hiyo jioni wakati tukijiandaa kumpelekea chakula, tulipata taarifa za msiba kwamba Simoni amefariki na wakati huo polisi walikuwa wanatafuta namna ya kuuondoa mwili huo,” alisema.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto alipoulizwa juzi juu ya tukio hilo alimtaka mwandishi kutoka kwenye kelele ili ampigie tena.
“Naona hapo ulipo kuna kelele, toka kwanza ndipo unipigie nitakujibu unachotaka,” alisema Muroto
Hata hivyo alipopigiwa hakupokea lakini alipotumiwa ujumbe alijibu kwa ufupi:  “Nalifuatilia utafahamishwa.”
Lakini jana alipoulizwa tena alisema hawezi kulizungumzia jambo hilo kwa kuwa alikuwa kwenye kikao.
Gondwe alisema walipofika hospitali ya mkoa wa Dodoma juzi, madaktari waliufanyia uchunguzi mwili wa Simon lakini wakasema hawawezi kutoa majibu ya moja kwa moja hadi vipimo vifanyike.
Alisema madaktari walisema hadi vipimo vipelekwe kwa mkemia mkuu Jijini Dar es Salaam na baada ya hapo ndipo watapelekewa majibu ya kilichosababisha kifo cha kijana huyo.
“Tunaomba uchunguzi wa awali wanagoma kutupa ndiyo maana tumeamua kususia mwili huo,” alisema Gondwe.
Msemaji huyo alisema ushirikiano wanaopewa na Polisi ni mdogo na unatoa taswira ya mashaka kwa pande hizo mbili na kwamba wanajadiliana kuona namna watakavyofanya au hatua zaidi wanazoweza kuchukua
Diwani wa Mtera, Amon Kodi alisema ni kweli kulikuwa na mgogoro huo.
“Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wakimlalamikia polisi huyo anayetuhumiwa kupiga na kuwatesa raia wanapokamatwa.” Alisema.


Comments

Popular Posts