Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

VIDEO-Kiboko azua taharuki kwa wakazi Tanga


Tanga. Baadhi ya wakazi jijini hapa, wakiwamo wagonjwa wamepatwa na taharuki baada ya kuuawa kiboko katika ufukwe wa Bahari ya Hindi karibu na Hospitali ya Bombo.
Kiboko huyo mwenye uzito wa kilo 1,500 na urefu wa futi nane aliuawa juzi katika ufukwe huo iliopo karibu na Hospitali ya Bombo.
Mnyama huyo kwa muda mrefu alikuwa akiwindwa na maofisa wa wanyamapori baada ya kubainika kuwa kuna viboko watatu wanaranda randa kando ya ufukwe huo.
Mgonjwa Adamu Hamis aliyelazwa wodi namba nane katika hospitali hiyo, alisema baadhi ya wagonjwa wanahofia kuvamiwa na viboko usiku.
“Mimi nafahamu kwamba viboko hutembea hata nchi kavu kutafuta nyasi na ni wanyama hatari kwa binadamu, kwa hiyo tumejawa na hofu huenda wakavuka uzio wakaingia eneo hili la hospitali,” alisema hamisi
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa aliwatoa hofu wagonjwa na wananchi akisema Serikali itahakikisha kiboko aliyebaki anauawa haraka kwa sababu ni rahisi kumpata.
“Kwa niaba ya Serikali nitumie fursa hii kuwatoa hofu wakazi wa Tanga na wagonjwa wa Bombo, msiwe na wasiwasi tutahakikisha kiboko aliyebaki anauawa haraka iwezekanavyo ili kurejesha hali ya amani katika fukwe zetu,” alisema Mwilapwa.
Ofisa Maliasili wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Aneny John Nyirenda alisema kiboko huyo aliyeuawa ni miongoni wa viboko watatu waliowahi kuonekana katika ufukwe wa bahari hiyo eneo la Rascazone, baadaye kutolewa kibali cha kuwaua.
“Huyo ni kiboko wa pili kuuawa katika ufukwe huu wa Rascazone, wa kwanza aliuawa wiki mbili zilizopita katika mashamba ya miwa na huyu ameuawa kando ya Hospitali ya Bombo,” alisema Nyirenda.
Alisema viboko hao wanadhaniwa kutoka katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani (Sanapa) kwenye Mto Ruvu ambako wamehifadhiwa.

Comments

Popular Posts