Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Wabunge kumuaga Kasuku Bilago Jumanne


Dar es Salaam. Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge kimesema kuwa, wabunge watauaga mwili wa mbunge wa Buyungu, (Chadema) Kasuku Bilago Jumanne, Mei 29, katika viwanja vya bunge.
 Taarifa iliyotumwa leo, Mei 27 na Ofisi ya Bunge imesema kuwa kuagwa kwa Bilago Jumanne, kumeafikiwa baada ya bunge, Chadema na uongozi wa familia kukubaliana.
“Baada ya waheshimiwa kutoa heshima zao za mwisho, mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Kakonko, Kigoma kwa mazishi,” imesema taarifa hiyo
Bilago amefariki jana, Mei 26 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akitibiwa

Comments