Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Zitto atangaza ushirikiano na Chadema Buyungu


Dar es Salaam. Unaweza kusema fukuto la uchaguzi katika Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma limeanza taratibu baada ya mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kuanza mkakati wa chinichini, akitaka vyama vya upinzani kushirikiana ili kuibuka na ushindi.
Leo Jumatano Mei 30, 2018, Zitto kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ameeleza kuwa yeye na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wamekubaliana kuwa watashawishi kuwepo na ushirikiano wa vyama vya upinzani katika uchaguzi huo.
Uchaguzi wa Buyungu utafanyika baadaye mwaka huu baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Kasuku Bilago kufariki dunia Mei 26, 2018.
“Kwa heshima ya mwalimu Bilago mimi na Mbowe  tumekubaliana kuwa tutashawishi kuwepo na democratic front (ushirikiano wa kidemokrasia) katika Jimbo la Buyungu,”amesema Zitto.
“Ama ACT itaunga mkono mgombea wa Chadema au Chadema itaunga mkono mgombea wa ACT Wazalendo. Tunataka kuweka mgombea mmoja anayekubalika na wananchi wa Buyungu na kufanya kampeni kwa pamoja mpaka ushindi.”
Amesema huo ni mwanzo wa harakati za kuwa na ushirikiano imara wa kidemokrasia dhidi ya ukandamizaji wa demokrasia nchini na hali mbaya ya maisha ya wananchi.
“Umoja wa zaidi ya vyama vya siasa ukihusisha vyama vya wafanyakazi, vyama vya wakulima, vyama vya wafanyabiashara na wananchi wengine,” amesisitiza mbunge huyo.

Comments

Popular Posts