Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Afisa Utumishi Mkuu wa TAKUKURU ametoa ushahidi kesi ya Mhasibu Mkuu Wao


Afisa Utumishi Mkuu wa TAKUKURU Ayoub Akida ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa aliyekuwa Mhasibu mkuu wa taasisi hiyo, Godfrey Gugai anayekabiliwa na kesi ya kumiliki mali za Bilioni 3.6 aliajiriwa June 11, 2001 kwa mshahara wa Sh. 120,940.

Akida ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati akiongozwa na Wakili wa Serikali, Pius Hilla akiwa ni shahidi wa kwanza upande wa mashtaka katika kesi hiyo.

Akida amedai kuwa ajira ya Gugai ilianza kama Afisa Mchunguzi daraja la 3 na kwamba ajira yake hiyo ilifikia ukomo August 2016.

“Baada ya kuajiriwa alikuwa akilipwa mshahara wa Sh.120,940 kwa mwezi na kwamba mbali na mshahara huo hakuwa na chanzo kingine cha mapato,” amesema Akida

Akida amedai kuwa kumiliki Mali siyo tatizo iwapo wangeziona katika fomu ya tamko la Mali na madeni isingekuwa lakini mali zake hakuzijaza kwenye fomu hizo za tamko la Mali na madeni.

Amedai kuwa baada ya Gugai kuajiriwa alithibitishwa kazini June 14,2002 na kwamba baadaye alipandishwa cheo na kulipwa mshahara wa kati ya Sh 1,382,450 na 1,521,830 na kwamba mbali na mshahara huo alikuwa akilipwa fedha ya umeme sh 150,000 na Sh 70,000 ya simu.

Shahidi hiyo amedai kuwa Mali zinazopaswa kujazwa kwenye tamko la Mali na madeni ni Mali zote zinazohamishika na zisizohamishika.

Aliongeza kuwa Gugai alichukuliwa hatua za kinidhamu na Mkurugenzi wa TAKUKURU baada ya kupata taarifa alikuwa na Mali nyingi maeneo tofauti tofauti nchini ikiwamo nyumba na viwanja.

Baada ya kueleza hayo, kesi imeahirishwa hadi July 10,2018 ambapo mashahidi wa upande wa mashtaka wataendelea kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

Mbali ya Gugai, washtakiwa wengine ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali.

Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decemba 2015.

Inadaiwa akiwa jijini Dar es Salaam kama mwajiriwa wa TAKUKURU alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh 3.6 bilioni ambazo hazilingani na kipato chake cha awali na cha sasa cha zaidi ya  Tsh.milioni 800,huku akishindwa kuzitolea maelezo. 



Comments

Popular Posts