Ajali mbaya imetokea mkoani Mtwara na kusababisha vifo vya watu watano na watatu kujeruiwa baada ya gari aina ya Toyota Noah walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka, kisha kuwaka moto.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ajali hiyo ilitokea jana saa 10 jioni katika kijiji cha Chingweje wilaya ya Nanyumbu mkoani hapa.
Kati ya waliofariki dunia ambao wametambulika ni dereva wa gari hilo Babuu Maroro
huku maiti nyingine wameshindwa kutambulika baada miili yao kuungua na moto.
Amesema majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika Hospitali ya Mkomaindo Masasi ni Daria Bushiri (30) mkazi wa Masuguru, Afkam Ling'ande (4) na Khalid Salum ambaye ni kondakta wa gari hilo.
“Lilivyoanza kuwaka moto, watu watatu walitoka salama ila watano walioshindwa kutoka waliungua, kati yao wawili wameungua vibaya na hawatambuliki. Watatu kidogo wanaweza kutambulika. Tunaomba ndugu jamaa kujitokeza kutambua miili ya marehemu ambayo imehifadhiwa katika hospitali ya Mkomaindo.”
Comments
Post a Comment