Viongozi wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Taifa wakiongozwa na M/kiti wa BAVICHA Taifa Patrick Sosopi, leo amekutana Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui ma kuweka mikakati ya kuwapigania vijana wanaokosa haki zao za msingi hasa za kupiga kura visiwani Zanzibar.
M/Kiti BAVICHA Taifa, Patick Ole Sosopi aliyevalia nguo nyeusi za chama, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Mhe.Nassor Ahmed Mazrui leo mapema alipozuru na ujumbe wake Ofisi kuu ya CUF Zanzibar.
Akiwa katika ziara huko Zanzibar, Sosopi ambaye ameongozana na wa Makamu M/kiti BAVICHA Zanzibar Zeudi Mvano na Katibu Mwenezi wa BAVICHA Taifa, Edward Simbeye, wamesema kwamba vijana wengi wanakosa haki zao kwakuwa tu ni wapinzani hivyo Masheha huwanyima barua za utambulisho ili kupata cheti cha kuzaliwa na hatimaye kitambulisho cha kupiga kura.
Pamoja na hayo viongozi hao wameweka mikakati mbalimbali ya kuimarisha UKAWA kwa upande wa visiwani ambapo kikao hicho kimeweka baadhi ya misimamo ya utekelezaji wa ushirikiano katika utendaji wa shuguli za Taasisi mbili za Vijana kwa maana ya JUVICUF na BAVICHA.
Mbali na hayo viongozi hao wamepanga namna ya kuwasaidia viongozi wakuu wa vyama vyao (CHADEMA, CUF) ili kuwapunguzia majukumu katika kazi za siasa na kuamsha ari mpya ya kusaka mabadiliko kuondokana na mkwamo wa kisiasa.
Comments
Post a Comment