Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Kubenea amhoji Kabudi sakata la makinikia

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea akichangia

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2018/2019, jijini Dodoma leo. 

Dodoma. Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amemtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kulieleza Bunge majadiliano baina ya Serikali na Kampuni ya Madini ya Acacia kuhusu makinikia yamefikia wapi.
Pia, amemtaka kuwaeleza Dola 190 bilioni zaidi ya Sh424 trilioni zinazopaswa kulipwa na Acacia zitapatikanani lini.
Akichangia bajeti ya wizara ya nishati ya mwaka 2018/19 leo Juni 1, 2018, Kubenea amesema inasikitisha amesoma kitabu cha bajeti cha waziri na cha kamati hakuna walipozungumzia makinikia.
“Sisi tulitegemea Bunge letu tupewe taarifa ya kina kuhusu mazungumzo kati ya Serikali na Acacia. Tuelezwe Sh424 trilioni ambazo ni Dola bilioni 190 tungepata lakini Bajeti nzima imekuja haijazungumzia na ripoti ya waziri hakuna kokote,” amesema Kubenea
“Kwa kuwa mmoja wa wajumbe ni Profesa Kabudi atuambie makinikia imefikia wapi, mchanga uliozuiwa bandarini upo, utakuwapo hadi lini, mchanga unasafirisha? Kiwanda cha kuchenjua kitajengwa lini?” amehoji
Kubenea amesema fedha hizo Sh424 trilioni zinapaswa kila Mtanzania apate matibabu, kuishi maisha mazuri kwa fedha hizo zinapatijkana lini?
 “Suala hili ni muhimu kuelezwa makinikia yako wapi. Mazungumzo yamefikia wapi, fedha zinapatikana lini ili tuipate. Tutajua kila wilaya, kata kitapata kituo cha afya, bajeti ya miaka kumi.”
“Fedha hizi ni nyingi sana na kama tumeibiwa, Serikali ijiangalie vizuri na ili kufikia malengo tusipige danadana tuimalishe Stamico itakayosimamia madini yetu,”amesema.

Comments