Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mahakama yamuachia huru mmiliki Jamii Forum



Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums, MaxenceMelo na Mwanahisa wa  mtandao huo, Micke William baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu.
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa aliwaachia huru washtakiwa hao leo Juni 1, baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka na kuona ushahidi huo hauna mashiko.
“Hakukuwa na ushahidi unaoeleza moja kwa moja wa barua hiyo ya kuwataka watoe taarifa za kampuni yao na ushahidi huo una mashaka?” amesema Mwambapa
Katika kesi hiyo Melo na mwenzake wanadaiwa kuzuia uchunguzi wa jeshi la polisi kwa kukataa kutoa taarifa za kampuni yao.
Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa,amedai kuwa baada ya usajili, kampuni hupewa taarifa za siri ambazo huwezesha mtu kuingia katika mtandao huo husika hivyo washtakiwa hao walikuwa na uwezo kuona taarifa kwenye mfumo wao.
Kishenyi amedai kuwa kufuatia jitihada hizo za Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum(ZCO) za kuwataka washtakiwa kutoa taarifa muhimu na wao kukataa walikamatwa na kufikishwa mahakamani.

Comments