Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Majaliwa awataka mawaziri kuchangamkia fursa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa tuzo ya


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa tuzo ya Balozi wa Amani na Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wabunge Wapenda Amani, Dk Thomas Walsh katika hafla ya kuzindua tawi la Tanzania la wabunge wapenda amani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, jijini Dodoma leo. Kushoto ni Spika wa Bunge, Job Ndugai.  
Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza mawaziri wa sekta zinazohusika na ufadhili unaotolewa na Chama cha Wabunge Wapenda Amani Duniani (UPF), kuwasiliana na viongozi wa shirikisho hilo ili kuchangamkia fursa za miradi mbalimbali.
Akizungumza leo Alhamisi Juni 28, 2018 katika uzinduzi wa tawi hilo nchini, Majaliwa amesema shirikisho hilo limekuwa likitoa misaada katika sekta za elimu, afya, kilimo na miundombinu mbalimbali.
“Nawaelekeza mawaziri wa sekta zinazohusika kufanya mazungumzo na viongozi wa shirikisho hili waliopo nchini ili kuchangamkia fursa zinazopatikana na uwepo wa shirikisho hilo,”amesema.
Majaliwa amesema ni vyema wabunge wakawaunga mkono wabunge wenzao ambao ni waanzalishi wa umoja huo nchini.
Amebainisha kuwa ili amani idumu katika ualisia wake, upendo na mapenzi lazima viwepo na kwamba Tanzania inaweza kunufaika katika misaada mbalimbali ikiwemo katika sekta za kilimo, afya elimu na miundombinu.
Hata hivyo, amesema ni mategemeo yake wabunge watakuwa vinara wa kusimamia amani na miradi itakayoanzishwa chini ya shirikisho hilo ili iweze kuleta tija kwa manufaa ya Taifa.
Amewataka kutumia fursa ya shirikisho hilo, kwa kuomba mafunzo ya wakulima na kwamba wanaweza kunufaika na mafunzo ya shamba la darasa la Kahawa kwasababu tayari shirikisho hilo lina shamba darasa Hawaii.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo nchini, William Ngeleja amesema shirikisho hilo limetenga Dola za Kimarekani bilioni 3 ambazo ni misaada isiyolipwa katika nchi 10 barani Afrika.
“Na sisi tutahakikisha kuwa tunatoa kipaumbele chetu ni katika fursa ambazo hazituongezei mzigo wowote Taifa,”alisema Ngeleja.
Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema wao kama Bunge wataendelea kuuunga
mkono umoja huo na kuwataka wabunge kuishi kwa mfano wa kupenda amani.
Katika uzinduzi huo umoja huo viongozi mbalimbali walikabidhi tuzo za
kutambua ushiriki wa wabunge katika kuanzishwa kwake ikiwa ni pamoja
na Majaliwa, Ndugai, Naibu Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson na
mwenyekiti wa umoja huo Mussa Ntimizi.

Comments

Popular Posts