Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mbunge CUF afunguka baada ya kutimuliwa bungeni

Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali akitii amri ya

Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali akitii amri ya Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya kumtaka kutoka kwenye ukumbi wa bunge leo wakati mjadala wa kupitisha muswada wa sheria ya fedha 2018, jijini Dodoma leo.  
Dar es Salaam. Saa chache baada ya mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali kutolewa nje ya ukumbi wa Bunge na Spika Job Ndugai, amesema chanzo ni uamuzi wake wa kutaka kueleza ukweli kuhusu suala la ushuru wa Korosho.
Bobali ametimuliwa nje ya ukumbi wa Bunge leo mchana baada ya kuibuka mvutano kati yake na Ndugai.
Akizungumza na MCL Digital kwa njia ya simu, Bobali amesema alisimama kupingana na maelezo yaliyokuwa yakitolewa na mbunge wa Siha (CCM), Dk Godwin Mollel kwa madai kuwa alikuwa akilipotosha Bunge.
“Nilishindwa kuvumilia ndio maana nilitaka kumpata taarifa Dk Mollel kuhusu ukweli wa masuala ya korosho. Sikupendezwa na maelezo yake wakati wa mjadala wa Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2018,” amesema.
“Hata hivyo nashukuru Mungu kwa kuniepusha kwa sababu sitaki kuwa sehemu ya watu watakaopitisha sheria hii ambayo naona inakwenda kuua zao la Korosho hasa kwa watu wa mikoa ya kusini,”amesema Bobali na kusisitiza kuwa sasa anarejea kwa wananchi wa jimbo lake kuwaeleza kuhusu suala la Korosho.



Comments

Popular Posts