Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Breaking News: Vitisho vyamng'oa diwani CUF Dar, ajiudhuru nafasi yake ikiwemo ya umeya ataja viongozi wa Chama


Diwani wa kata ya Vingunguti kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi CUF ambae pia ni naibu meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam Omary Kumbilamoto amejiudhuru nafasi yake majira ya rasmi leo. 

Akizungumza na wahanahabari Kumbilamoto amesema kuwa amechukua uamzi huyo kutokana na vitisho anavyopewa na viongozi wa chama hicho pindi amepoungana na viongozi wa serikali katika kutekeleza majukumu ya kuwatumikia wananchi. 

"Nimejivua uanachama wa CUF na nafasi zangu zote ndani ya chama ikiwemo ya udiwani katika kata ya Vingunguti pia unaibu meya wa manispaa na nimechukua hatua ili kulinda na kutetea maslahi ya wananchi ninaowatumia hivyo ili niendelee kuteleza majukumu yangu ipasavyo najivua ili kuunga mkono jitihada za rais Magufuli na viongozi wote Serikali kwa ujumla" amsema Kumbilamoto. 

Ameongeza kuwa ndani ya chama cha wananchi Cuf kuna mgogoro ambapo amefananisha mgogoro kuwa ni sawa na ule wa Israil na Palestina kwani hauna suluhu, hivyo mara nyingi nimekuwa nijikita zaidi kusaidia kutatua changamoto za wananchi lakini viongozi wananitishia kunivua uanachama hivyo ni maamuzi magumu niliyoyafanya kwa wananchi wangu ila imenilazimu kufanya hivyo ili niwe huru kwasasa 

Aidha Rais wetu mpendwa amekua na ushawishi mkubwa kwa kuteleza changamoto hususani katika kuleta maendeleo nchini ikiwemo ujenzi wa fly over ya tazara, kununua ndege kwani tumekuwa tukishudia nchi za wenzetu wakiwa na vitu kama hivi lakini kwa sasa tuanaona hapahapa kwetu hivyo nampongeza kwa jitihada zake. 

Ameongeza kuwa katika miaka miwili ya udiwani ametekeleza ahadi mbalimbali ikiwemo kununua Ambulance ya wagonjwa kukarabati hospitali, lakini cha kushangaza kipindi cha masika wananchi walipata madha lakini hajawahi kuona kiongozi yeyote wa chama cha CUF akienda kusaidia au kuzungumza chochote zaidi ya Mkuu wa Mkoa na Wilaya ambao walikwenda kuona na kuwasaidia.

Comments

Popular Posts