Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mahakama Yamuonya Mbowe


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imempa onyo  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe kwa kutohudhuria mahakamani mara mbili  katika kesi ya uchochezi inayomkabili yeye na wenzake nane. Ameambiwa iwapo atarudia tena kutofika mahakamani kwa sababu ambazo hazina msingi basi dhamana yake itafutwa.



Onyo hilo limetolewa leo Julai 31 na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH).



“Mwambieni asiendelee tena na huo mchezo aheshimu masharti ya dhamana na akirudia tena mahakama itamchukulia hatua ikiwamo kumfutia dhamana yake na kutaifisha fungu la dhamana ambalo ameliweka”.



Aidha Hakimu Mashauri ameondoa kumbukumbu barua zilizowasilishwa na wakili wa utetezi, Hekima Mwasipu ambazo ni nakala ya kusudio la kukata rufaa dhidi ya uamuzi uliotolewa katika maombi ya marejeo namba 126,2018 ya Mahakama Kuu na mwenendo wa maombi hayo.



Amesema, ataweka kumbukumbu hiyo pale wahusika watakapoyafikisha mahakamani kwa mujibu wa sheria. Kesi hiyo imepangwa Agosti 2,2018 kwa ajili ya washtakiwa kusomewa (PH).



Mapema wakili wa utetezi, Hekima Mwasipu alieleza mahakamani kuwa Mbowe hayupo lakini mdhamini wake yupo. Mdhamini wa Mbowe, ameileza mahakama kuwa amefanya mawasiliano na mshtakiwa (Mbowe) na amemueleza kuwa amekwama kwenye foleni.



Baada ya kutolewa kwa Maelezo hayo, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliiomba mahakama kumuingiza Mbowe kwenye kumbukumbu zake kuwa hiyo ni Mara ya pili mfululizo mshtakiwa ahudhurii kesi mahamani bila ya kutoa sababu za msingi.



“Julai 25, mwaka huu Mbowe hakufika mahakamani na mdhamini alieleza kuwa ameharibikiwa na gari akitokea Arusha, Leo amekwama katika foleni.



Naomba mahakama itoe onyo kwa washtakiwa kuheshimu masharti ya dhamana na kufika mahakamani kwa wakati.” Amedai Nchimbi.


Mahakama Yamuonya Mbowe

Wakili Mwasipu amedai mahakamani hapo kuwa, pamoja na kesi hiyo kupangwa kwa PH leo lakini mawakili wanaoiendesha kesi hiyo, Peter Kibatala yupo Mahakama Kuu na Jeremiah Mtobesya yupo Mwanza wameomba kesi iahirishwe hadi Agosti 2,2018 Saa 5 asubuhi watakuwepo.



Pia amewasirisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa mahakamani hapo na barua ya kuomba mwenendo wa maombi ya marejeo Mahakama Kuu.



Hata hivyo, wakili Nchimbi aliiomba mahakama kwa sasa isipokee maombi ya taarifa hiyo hadi pale yatakapofikishwa kwa kufuata utaratibu na msingi wa sheria.



Washtakiwa waliokuwepo mahakamani ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na  mbunge wa bunda, Esther Bulaya.



Wengine ni mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji.



Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.

Na Ripote wa Globu ya Jamii 

Comments

Popular Posts