Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete
Pwani. Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete amesema sababu ya wapinzani kuhamia chama tawala inatokana na mambo mazuri yanayofanywa Serikali ya Awamu ya Tano.
Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 31, 2018 kupitia ukurasa zake za mitandao ya kijamii.
Amesema kutokana na wimbi hilo la wapinzani kuhamia CCM wa kulaumiwa ni Serikali hiyo kutokana na kufanya mambo ya uhakika yanayowavutia.
Wabunge wengine wa Chadema waliotimkia CCM ni Mwita Waitara na Dk Godwin Mollel. Dk Mollel alipitishw ana CCM kuwania tena ubunge katika jimbo la Siha na kuibuka mshindi.
Kupitia ukurasa wake Ridhiwani amesema, “kama hauwezi pambana ungana nasi karibuni nyumbani kumenoga.
Comments
Post a Comment