Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri wa Afya Awajia Juu Wanaume "Likizo Ya Uzazi Kwa Wanaume Si Ya Kunywa Pombe’'

Waziri wa Afya: Awajia Juu Wanaume "Likizo Ya Uzazi Kwa Wanaume Si Ya Kunywa Pombe’'

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka wanaume kutoitumia likizo ya siku tano ya uzazi kwa wanaume kwenda kunywa pombe.

Aidha, amesema ataifuta likizo hiyo kwa wanaume endapo atajiridhisha haina manufaa na inatumika ndivyo sivyo.

Akizungumza kuhusu Wiki ya Unyonyeshaji itakayoanza kesho hadi Agosti 8, mwaka huu, Waziri Ummy amesema likizo hiyo ni kwa ajili ya kumsaidia mama anapokuwa amejifungua na si vinginevyo.

“Likizo ya uzazi kwa wanaume si ya kwenda kunywa pombe, lakini wapo wanaume wanachukua likizo na nyumbani hawaonekani, nitafanya utafiti kuangalia iwapo ina manufaa kama hakuna tutaifuta,” amesema.

Comments

Popular Posts