Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

ACT-Wazalendo wamjibu Kangi Lugola sakata la Zitto kujisalimisha polisi

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho,Ado Shaibu 
Dar es Salaam. Chama cha ACT-Wazalendo kimemtaka kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe kuendelea na majukumu yake kama kawaida kwa kuwa agizo lililotolewa na Waziri wa mambo ya Ndani Kangi Lugola halina nguvu kisheria.
Jana Lugola alimtaka Zitto kujisalimisha kwa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi kwa kile kilichoelezwa alitoa maneno ya kichochezi wakati wa mkutano wa hadhara kati yake na Mbunge wa Kilwa Kusini(CUF), Seluiman Bungara 'bwege'.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho,Ado Shaibu ametoa kauli hiyo leo Jumatano Agosti Mosi 2018 wakati akizungumza na wanahabari.
Amesema wanasheria wa chama wamelipitia kwa undani tamko hilo la Lugola na kujiridhisha kuwa lina makosa na halina nguvu kisheria.
"Wanasheria wa chama wamejiridhisha pasipo shaka na kugundua kuwa Lugola amekulupuka kutoa tamko lile.Lugola katumia siasa kutoa tamko lile na siyo kufuata sheria.
“Zitto akaitwa kisheria ataenda kuripoti polisi na hatuna sababu ya kuogopa.Zitto ni kiongozi mbunge akiitia wito huu wa Lugola atakuwa hajiheshimu, "amesema Shaibu.
Shaibu amesema hakuna kosa lolote ambalo Zitto amelitenda katika mkutano ule, lakini Lugola amekuwa na makeke katika kutoa matamko yake.
“Yaani tumetesti mitambo mara moja tu, pale Kilwa kwa kumpandisha jukwaani Zitto imekuwa nongwa watu wanalipuka? Hatuwezi kuvumilia hali hii,"amesema.

Comments