Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Fred Lowassa Ajiondoa Kuwania Ubunge Monduli


Kada wa Chadema, Fred Lowassa leo Agosti 15 amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha wanaowania kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge jimbo la Monduli.

Baada ya kujiondoa, Chadema kimempitisha diwani wa kata ya Lepurko, Yonas Masiaya Laizer kuwania ubunge wa jimbo hilo.

Fred, ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa alichukua fomu ya kuwania ubunge jimbo hilo wiki iliyopita.

 Aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Julius Kalanga, alijiuzulu uanachama wa Chadema na ubunge na kuhamia CCM. Kalanga ameshateuliwa na CCM kugombea ubunge jimbo hilo.

Akizungumzia uamuzi wa Fred, katibu wa Chadema mkoa wa Arusha, Amani Golugwa alisema baada ya kushauriana, vikao vya uteuzi vilikubali kuondoa jina lake.

"Ni kweli nathibitisha kuwa ameomba kwa sasa si wakati muafaka licha ya kuwa alionesha nia awali na wananchi wengi walimuunga mkono, hivyo chama kimekubali maombi yake na kimempitisha mgombea mwingine,"amesema Golugwa.

Comments

Popular Posts