Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Kafulila ala kiapo mara mbili

Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Songwe, David

Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Songwe, David Kafulila 
Dar es Salaam. Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Songwe, David Kafulila amejikuta akila kiapo mara mbili baada ya kukosea kusimama, leo Agosti 1 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kafulila, aliyewahi kuwa mbunge wa Kasulu, (NCCR-Mageuzi) aliteuliwa na Rais John Magufuli wiki iliyopita.
Kafulila alionekana kusimama akiwa ameelekea upande wa kushoto na ndipo alipoelekezwa kumwelekea Rais.
Katibu Mkuu kiongozi, John Kijazi alipoona kasoro hiyo, alimwelekeza Kafulika kumwelekea Rais na akaapa upya.
Mbali na Kafulila, Jill Maleko Katibu tawala mkoa wa Mtwara naye alitakiwa kurudia kiapo chake.

Comments