Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Lukuvi awakomalia wapima ardhi kuacha ujanjaujanja



Dodoma. Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amewataka wapima ardhi wa wizara na wa binafsi kuacha ujanjaujanja na wizi katika masuala ya upimaji.
Pia, amewafananisha wapima ardhi wanaofanya kazi kwa ujanja ujanja na wanaopima nyama na kisha kuondoka na maini.
Lukuvi aliyasema hayo jana wakati akizungumza na maofisa ardhi kwenye mafunzo ya wapimaji wa Serikali pamoja na wale wa binafsi.
Alisema amebaini mtandao wa wapima ardhi ambao hata wakipewa eneo la makaburini kupima ni lazima watajitengea viwanja.
“Ila na nyie muache ujanja na wizi katika kupanga maana nimeshaanza kujua wale wajanjawajanja kuna wilaya zao nawapeleka, mna mtandao wenu yaani hakuna mpima (ardhi) ambaye amehama wilaya moja akawa hana viwanja hata ukimpeleka usiku mmoja ataficha viwanja kama vitatu,” alisema. Hata hivyo, Lukuvi alisema Serikali haitamvumilia mpima ardhi atakayekwenda kinyume na maadili ya kazi hiyo.
Alisema kuna mpango wa kufanya upimaji wa ardhi nchi nzima ambapo kwa sasa wanafanya majaribio katika Mkoa wa Morogoro na unaenda vizuri.
Lukuvi ambaye ni mbunge wa Isimani, alisema wanataka kila mtu anayejenga mjini au wenye nyumba sehemu hizo wawe na hati kama sehemu ya uwezeshaji binafasi kwa wananchi ili waweze kupata mikopo benki pamoja na kuiwezesha Serikali kwa mapato ya kodi.
Akizungumza kwa niaba ya wapima ardhi, Robert Canon alisema mafunzo hayo yatawasaidia kutumia vifaa hivyo kwa ufasaha na ufanisi, na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili viweze kudumu kwa muda mrefu.
Alisema watatoa mchango wao wa upimaji ardhi kwa ajili ya kuongeza pato la Serikali na kuwezesha ukuaji wa uchumi wa viwanda, kwa kuwa ardhi isipopimwa ni vigumu kupata wawekezaji.

Comments

Popular Posts