Skip to main content

Featured

Maombolezo: Hii ndiyo Hali Ilivyo Tanzania Bendera Yapepea Nusu Mringoti

Agizo la Rais John Magufuli la Bendera ya Taifa kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 22 kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mkoani Mwanza limetekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

MUFTI MKUU SHEIKH ZUBERI AMTEMBELEA KIGWANGALLA NA KUMFANYIA DUA MAALUMU KATIKA TAASISI YA MIFUPA (MOI)



Na Andrew Chale
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh, Abu Bakari Zuberi  leo Agosti 31,2018 amemtembea na kumuombea dua maalum Dkt Hamisi Kigwangalla ambaye anapata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI akiuguza majeraha ya mkono aliyopata katika ajali iliyotokea Agosti 4, mwaka huu Mkoani Manyara. 

Mufti, Sheikh Zuberi  aliambata na Mjumbe wa Halmashauri Kuu BAKWATA, Sheikh  Yusuph Hassan Tonge ambapo kwa pamoja wameweza kuendesha dua maalum ili kupona haraka majeraha yake.

“Nimetoka Makka kwenye hijja tumekuombea dua. Nimerejea nikaona nije kukuona na pia kukuombea dua ili upone haraka.”  Alisema Mufti, Sheikh Zuberi.

Mbali na dua, pia Mufti, Sheikh Zuberi ameweza kumpongeza Dkt. Kigwangalla kwa juhudi zake za kazi katika Wizara yake hiyo.

Aidha, Dkt. Hamisi Kigwangalla amemshukuru Mufti Mkuu, Sheikh Zuberi  pamoja na BAKWATA kwa kuendelea kumuombea dua ambapo pia aliwaeleza kuwa kwa sasa hali yake inazidi kuimarika huku akisubiria ripoti za Madaktari.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa Taasisi ya MOI, Fiderisi Minja ambaye aliwapokea wageni hao, amesema kuwa Madaktari Bingwa na Wauguzi wanaendelea kutoa tiba bora  kwa wagonjwa wote wanaofika kufanyiwa tiba katika taasisi hiyo.

Dkt. Kigwangalla alihamishiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI tarehe 12/08/2018 baada ya kupata matibabu ya awali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kwa sasa bado anaendelea na tiba kuuguza mkono wake wa kushoto.

Comments

Popular Posts